Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge wa Afrika Kusini asimamishwa kazi kwa matamshi ya kibaguzi

Mbunge Wa Afrika Kusini Asimamishwa Kazi Kwa Matamshi Ya Kibaguzi Mbunge wa Afrika Kusini asimamishwa kazi kwa matamshi ya kibaguzi

Thu, 20 Jun 2024 Chanzo: Bbc

Chama cha Democratic Alliance (DA) kimemsimamisha kazi mbunge mmoja baada ya video ya zamani kuibuka tena mtandaoni ikimuonesha akitoa lugha ya kibaguzi dhidi ya watu weusi.

Awali Renaldo Gouws alidai kuwa ni video iliyothibitishwa na akakanusha lakini taarifa iliyotolewa na DA siku ya Alhamisi ilisema ni "halisi na si ya uwongo".

Katika video hiyo Bw Gouws, ambaye aliapishwa bungeni chini ya wiki moja iliyopita, anatumia lugha ya kibaguzi kwa Waafrika Weusi mara kwa mara.

DA ambayo sasa ni sehemu ya serikali ya umoja wa kitaifa ilisema Bw Gouws atakabiliwa na "mashtaka ya kinidhamu".

Chanzo: Bbc