Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge mwenye simu 19; "Zote nazitumia kila siku"

Mbunge Simuu Mbunge mwenye simu 19; "Zote nazitumia kila siku"

Sat, 9 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Jimbo la Kesses nchini Kenya, Mishra Swarup mwenye asili ya Kihindi amekiri ni kweli anamiliki simu 19 za mkononi na zote anazitumia katika matumizi ya kila siku na kwamba kila moja ina nafasi yake muhimu katika shughuli zake za kutunga sheria, ujasiriamali na familia.

“Nina simu 19 sasa, na ninazitumia zote, nyingine ni za biashara, nyingine ni kwa ajili ya Wananchi na nyingine ni za uhusiano wangu wa kisiasa na kikazi.

"Ninawaasiliana na watu wangu waliopo China, India, Zambia na Congo, nina simu kwa ajili ya mama yangu, Baba yangu, Rais wangu, Naibu Rais wangu, Raila Odinga, mimi na mke wangu pia."

Mishra ambaye anatetea kiti chake cha Ubunge kama Mgombea huru kwenye uchaguzi mkuu wa Kenya utakaofanyika hapo Agosti, mwaka huu alionesha pia iPhone yake ambayo anadai imetengenezwa kwa dhahabu safi na almasi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live