Mbunge wa Jimbo la Mumias Mashariki, Peter Salasya amekamatwa na Jeshi la Polisi nchini Kenya, kwa kosa la kumshambulia na kumsababishia maumivu Diwani (MCA) wa Kakamega, Peter Walunya Indimuli.
Tukio hilo la aina yake, lilitokea kwenye shughuli za mazishi, ambapo kulitokea hali ya kutoelewana kati ya wawili hao, kabla ya mbunge huyo kumrukia na kumzaba kofi diwani huyo.
Salasya alikamatwa juzi jioni, Januari 12, 2024 na baadaye kuachiwa kwa dhamana ya shilingi 50,000 za Kenya (takribani shilingi 790,000 za Tanzania).
Bado haijafahamika ni nini hasa kilichosababisha mbunge huyo afanye kitendo hicho ambacho ni kinyume na maadili ya uongozi.