Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge aliyeunga mkono Muswada wa fedha Kenya aeleza alivyookolewa na Gen Z

Mbunge Aliyeunga Mkono Muswada Wa Fedha Kenya Aeleza Alivyookolewa Na Gen Z Mbunge aliyeunga mkono Muswada wa fedha Kenya aeleza alivyookolewa na Gen Z

Fri, 28 Jun 2024 Chanzo: Bbc

Askofu na Mbunge Mteule Jackson Kosgei Jumanne aliachwa na wenzake wakati waandamanaji wa Gen Z walipovamia bunge na kuteketeza eneo moja.

Kulingana na gazeti la The Star, Mbunge huyo mwenye matatizo ya kimwili alikumbuka matukio ya Jumanne, Juni 25, wakati wa maandamano ya #OccupyParliament kupinga Muswada wa Fedha wa 2024.

Wabunge wengine walilazimika kukimbilia usalama wao wakati vijana wa Gen Z walipovunja uzio wa bunge na kuingia kwa nguvu licha ya vizuizi vya usalama vilivyokuwa vimewekwa.

Takriban watu 5 waliuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa wakati polisi walipowafyatulia risasi waandamanaji.

Mbunge huyo aliyezungumza na runinga moja mjini Nairobi na kunukuliwa na gazeti la The Star alisimulia siku hiyo akihofia usalama wake.

Hata hivyo, alinusurika baada ya umati wa Vijana hao kumhakikishia kuwa hawatamdhuru."Licha ya ya kwamba ilikuwa katika hali ya hasira, walionyesha sura ya kibinadamu. Walipoingia walisema mzee tunakujua, ulikopiga kura, na tunakujua kama mtu mwema," alisimulia.

Katika video zilisosambaa mtandaoni, mbunge huyo alisindikizwa nje na kikundi kilichomuhakikishia usalama.

"Kwa hiyo walisema suala la wapi ulipiga kura na kadhalika sio hoja. 'tunataka kukusaidia kwa sababu kinachoweza kutokea hapa kinaweza kisiwe kizuri kwako," Kosgei alisema.

Chanzo: Bbc