Chinyere Igwe, Mwanasiasa wa upinzani wa Chama cha PDP ambaye pia ni Mbunge anashikiliwa kwa kutaka kutakatisha Dola 500,000 (Tsh. Bilioni 1.16) zilizokutwa kwenye Gari lake muda mfupi kabla ya Uchaguzi Mkuu unaofanyika leo Februari 25, 2023.
Polisi wamesema mtuhumiwa alikuwa na orodha ya majina ya Watu ambao alitakiwa kuwapatia Fedha hizo. Inadaiwa 40% ya Raia wa Nigeria hawana akaunti za Benki, hivyo wanategemea Fedha taslimu kwa matumizi ya kila siku.
Hivi karibuni, Nigeria ilizindua noti mpya ambazo bado mzunguko wake haujawa mkubwa, inadaiwa hilo linawapa wakati mgumu Wanasiasa wanaotaka Fedha nyingi kununua kura na kulazimika kutumia Dola.