Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge akiri hadharani: Mimi na wenzangu tulimsaidia Kenyatta kuiba kura za Urais

Kuria Jk Moses Kuria

Mon, 4 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Gatundu Kusini, Moses Kuria amefika mbele ya Tume Huru Inayosimamia Mipaka ya Uchaguzi nchini Kenya (IEBC), ili kutoa maelezo baada ya kukiri hadharani kwamba yeye na baadhi ya wabunge wenzake walimsaidia Rais Uhuru Kenyatta kuiba kura mwaka wa 2017.

Kuria alitoa madai hayo wakati wa Kongamano la Kitaifa la Wajumbe wa UDA wiki chache zilizopita.

"Mheshimiwa Waiguru, Rigathi, Kimani Wamatangi, Muthomi Njuki, Mithika Linturi, Alice Wahome, Faith Gitau... tulimsaidia Uhuru kushinda uchaguzi na sisi ndio tuliomuibia. Kikosi chote kilichohusika kumueka Uhuru mamlakani kiko hapa,” Kuria alidai wakati huo.

Kufuatia matamshi hayo, IEBC ilisema itamchunguza kiongozi huyo wa Chama Cha Kazi, kwa kukiri mdai yanayokwenda kinyume na maadili. Baada ya kukamilisha uchunguzi huo, IEBC ilimtaka Kuria kufika mbele ya Kamati ya Nidhamu ya ili kujitetea siku ya Jumatano, Machi 30.

Muda mchache kabla ya kufika mbele ya kamati, Kuria alisema kuwa alifika kwenye ofisi za IEBC ili kufungua 'servers'. "Nimefika IEBC ili nifungue servers," Kuria alidai.

Haikubainika ni nini Mbunge huyo alichokuwa akimaanisha kwamba angefungua 'servers' hapo IEBC, ila tamko hilo hutumika sana na Wakenya kumaanisha kufichua ukweli kuhusu suala fulani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live