Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge afichua Kanisa waumini hushiriki ngono bila kinga

Wamaua Mbunge afichua Kanisa waumini hushiriki ngono bila kinga

Tue, 20 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Maragua Bi Mary wa Maua Jumapili, Juni 18, 2023 alidai kuwa anajua kanisa moja Jijini Nairobi lenye matawi nchini ambapo kuanzia saa nane mchana huwa ni wakati wa washirika kujamiiana.

“Kuanzia saa nane mchana, washirika huwa wanatoa nguo na kubakia uchi wa mnyama kisha wanashiriki ngono ndani ya kanisa,” akasema katika kanisa la Pentecostal Evangelistic Fellowship of Africa (PEFA) lililoko katika mtaa wa Kamahuha, Kaunti ya Murang’a.

Mgeni wa heshima katika kanisa hilo alikuwa Waziri wa Usalama wa Ndani Profesa Kithure Kindiki.

Bi Wa Maua alizua msisimko wakati aliambia Prof Kindiki awaze na awazue hali hiyo ingekuwa ndiyo inatekelezwa katika kanisa la PEFA.

“Waziri tafakari hili…Saa nane itupate hapa na tuamrishwe kutoa nguo tubaki uchi. Lile tunda la Adamu na Hawa sasa tuanzane nalo hapa.

“Mimi ikiwa nimekuwa nikikutamani…Na wewe na huyo, yule…Matunda yaliyo hapa sasa yawe ni yetu kumegana,” akasema, akisababisha washirika wa kanisa kuangua kicheko.

Bi wa Maua alimtaja pasta wa kanisa hilo kuwa mfano wa Ibilisi katika himaya ya Jehanamu “na ndiyo sababu tunaunga mkono kikamilifu msako dhidi ya makanisa yanayoshirikisha uhaini wa kidini.”

Bi Wa Maua aliongeza kuwa sheria za kudhiibiti imani hapa nchini ni lazima ziundwe bungeni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live