Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge Osoro Ajibizana na Mkazi Aliyemuomba Msaada Facebook

39e3d120561f385e Mbunge Osoro Ajibizana na Mkazi Aliyemuomba Msaada Facebook

Thu, 1 Apr 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Osoro alikuwa amechapisha ujumbe mitandaoni kumuomboleza mbunge wa Kiambaa Paul Koinange

- Mmoja wa wafuasi wake kwa jina Cleousphus Machogu, katika maoni yake alimkumbusha mbunge huyo hukuhusu msaada aliomuomba

- Machogu, ambaye inasemekana ni mwalimu, alilalamika kuwa mbunge huyo mshirika wa Tangatanga hakuwa akijibu ujumbe wake

Mbunge wa Mugirango Kusini Sylvanus Osoro amejibizana na mmoja wa wakazi wake alimuomba msaada kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Osoro alikuwa amechapisha ujumbe mitandaoni kumuomboleza mbunge wa Kiambaa Paul Koinange laki mmoja wa wafuasi wake kwa jina Cleousphus Machogu, alimkumbusha mbunge huyo hukuhusu msaada aliomuomba awali.

Machogu, ambaye inasemekana ni mwalimu, alilalamika kuwa mbunge huyo mshirika wa Tangatanga alikuwa akipuuza jumbe alizokuwa akimtumia.

Hata hivyo mbunge huyo hakusita kumjibu akimuuliza ni vipi alifika katika afisi yake kumuomba amsaidie kupata uhmisho kutoka Voi.

Mtamshi ya mbunge huyo yaliwaudhi baadhi ya watu mitandaoni. Haya ni baadhi ya maoni yao;

Kwingineko afisa wa polisi Sammy Ondimu Ngare alimfokea shabiki aliyedai polisi walisajiliwa katika huduma ya maafisa wa taifa baada ya kufeli mitihani ya kitaifa.

Ngare alikuwa akiwasiliana na wafuasi wake Facebook akiwataka kumpa maoni ya jinsi polisi watakavyotekeleza amri ya kutotoka nje nyakati za usiku iliyotangazwa na Rais Uhuru Kenyatta Ijumaa, Machi 26.

Hata hivyo shabiki laiyejulikana kama Cynthia Chekatah alidai maafisa wa polisi wamejaa kiburi pasi na kuja kwmaba walisajiliwa katika kikosi baada ya kufeli mitihani.

Afisa huyo ambaye pia ni msanii alimfokea Chekatah kwa wazo lake duni kuwahusu polisi.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke