Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge Moses Kuria akamatwa usiku kwa Kuvunja sheria za COVID-19

8ed36b2fd4d8ba31 Mbunge Moses Kuria akamatwa usiku kwa Kuvunja sheria za COVID-19

Tue, 13 Apr 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Kuria kupitia ukurasa wake wa Facebook alidai kuwa anazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Karuri, kaunti ya Kiambu

- Mbunge huyo anadaiwa kukiuka sheria za kudhibiti kuenea kwa COVID-19 baada ya kufanya mkutano ndani ya hoteli moja eneo la Northern Bypass

- Kuria anatazamiwa kufikishwa kortini hii leo Jumanne, Aprili 13

Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria amekamatwa kufuatia msako wa polisi usiku mnamo Jumatatu, Aprili 12.

Akithibitsha habari hizo, Kuria kupitia ukurasa wake wa Facebook alidai kuwa anazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Karuri, kaunti ya Kiambu.

Duru zimedokezea kuwa Mbunge huyo alikiuka sheria za kudhibiti kuenea kwa COVID-19 baada ya kufanya mkutano ndani ya hoteli moja eneo la Northern Bypass.

Kulingana na habari zilizofikia Tuko.co.ke, mkutano huo uliandaliwa ili kujadili uchaguzi mdogo ujao katika bunge la Juja ambapo Kuria amemteua mgombea wa chama chake cha People Empowerment Party.

Picha zilizochapishwa na Kuria zinamuonyesha akiwa kwenye kituo cha polisi pamoja na baadhi ya wafuasi wake.

Kukamatwa kwa Kuria kulikujia saa chache baada ya mgombea wa chama hicho ambaye ni mke wa George Koimburi kukamatwa.

"Waoga wamemkamata mke wa Mheshimiwa George Koimburi, mgombea wa PEP kwa kiti cha Juja. Atafikishwa kortini kesho Thika. Lakini hakuna kitu ambacho kitazuia mabadiliko. Tukutane Thika asubuhi," alisema mbunge huyo.

Haya pia yanajiri baada ya Kuria kuomba Shirika la Fedha Duniani (IMF) kubadilisha mtindo wake wa kufanya biashara na Kenya.

Kuria alisema kutokana na ufisadi, ni vigumu kufuatilia namna mkopo wa shirika hilo umekuwa ukitumika akipendekeza badala ya kutoa mkopo ni vyema kupea Kenya chanjo.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke