Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge Joshua Kutuny, Wenzake Wazuiwa Kuzungumza Mazishini

2ce213c4633496c0 Mbunge Joshua Kutuny, Wenzake Wazuiwa Kuzungumza Mazishini

Sun, 28 Mar 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Robin alizikwa nyumbani kwao eneo bunge la Cherang'any Jumamosi Machi 27

- Mbunge wa eneo hilo Joshua Kutuny na wenzake waliohudhuria hawakuruhusiwa kuhutubia waombolezaji

- Robin alimwacha mjane na watoto watatu huku familia yake ikisema kifo chake ni pigo kubwa

Wanasiasa walizuiwa kuzungumza wakati wa mazishi ya aliyekuwa mtangazaji wa redio Citizen Robin Njogu.

Njogu alikuwa akizikwa nyumbani kwao Trans Nzoia katika eneo bunge la Cherang'any Jumamosi Machi 27.

Safari yake ya mwisho ilihudhuriwa na mamia ya waombolezaji, marafiki, familia na wafanyakazi wenzake kutoka Royal Media Services.

Wanasiasa Chris Wamalwa, Caleb Kositany na mbunge wa eneo hilo Joshua Kutuny walihudhuria pia.

Hata hivyo, wanasiasa hao hawakuruhusiwa kutoa rambirambi zao kwa waombolezaji familia ikisema haitaka siasa wakati wa kumuaga mpendwa wao.

Mjane wa Njogu, Carol Robin, aliwaacha wengi kwa majonzi baada ya kusimulia walivyopendana na penzi lao kushika.

Alisema wawili hao walikutana katika chuo anuwai cha mafunzo ya uanahabari KIMC jijini Nairobi na ndume huyo kumtamani.



"Alianza kuniaandama lakini nilikuwa namhepa kwa sababu nilikuwa nimeonywa kuhusu ndume kama hao. Baadaye aliendelea kunifuata na wakati mmoja akanikopa shilingi mia moja, na aliponirudishia urafiki wetu ukaanza," alisema Carol.

Alisema Njogu alikuwa ni mtu aliyempenda sana na kwa wakati mmoja gari la kampuni aliyokuwa akifanyia kazi hapo awali liliibwa baada ya Njogu kuliacha limeegeshwa Jericho ili wakutane.

"Wezi walikuja na kuagiza dereva waondoke, sijui aliporudi kazini alielezea ni vipi walikuwa Jericho wakati walifaa kuwa wakifuatilia taarifa kwingine," alisema Carol.

Mwandishi huyo hapo awali alifanya kazi na Capital FM kutoka 1999 hadi 2012 kama mhariri wa habari kabla ya kuhamia Nation Media Group.

Mnamo mwaka wa 2015, alijiunga na Royal Media Services kama mkurugenzi mkuu, ambapo alisimamia vituo 13 vya redio.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke