Aliyekuwa Mbunge wa Malindi nchini Kenya, Aisha Jumwa amejibu maswali ambayo yanazingira imani yake ya kidini alipofika mbele ya kamati ya bunge kuhusu uteuzi.
Jumwa ambaye alifika mbele ya kamati hiyo kupigwa msasa baada ya kuteuliwa na Rais William Ruto kwa wadhifa wa Waziri wa Huduma ya Umma, alisema kuwa yeye ni Mkristo.
Kwa mujibu wa Jumwa, alizaliwa na kukulia katika dini ya Kiislamu na kupewa jina la Kiislamu lakini amebadili dini na sasa ni mfuasi wa Kristo.
"Ndio, nilibadili na kuwa Mkristo na Aisha ni jina la Kiislamu. Nilikuwa Muislamu. Jina langu lilikuwa," Jumwa alisema.
Waziri huyo mteule amesema kuwa licha ya kubadili dini aliamua kubaki na jina lake la Kiislamu.
"Mimi sasa ni Mkristo, mwenye imani sana. Mimi ni Muislamu kwa jina na Mkristo kwa imani," Jumwa aliongeza.