Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbu wa Malaria kutoka Asia ahamia Afrika

Mbu Wa Malaria Kutoka Asia Ahamia Afrika Mbu wa Malaria kutoka Asia ahamia Afrika

Wed, 2 Nov 2022 Chanzo: BBC

Wanasayansi wanasema kwamba aina vamizi ya mbu anayeeneza malaria kutoka Asia imeenea hadi Afrika, ambako ni tishio hasa kwa wakazi wa mijini.

Barani Afrika, ambapo vifo vingi vya Malaria duniani hutokea, ugonjwa huu huenezwa zaidi na mbu maalumu kwa maeneo ya vijijini.

Lakini aina ya mbu wa Anopheles stephensi, ambaye ndiye anayehusika na visa vingi vinavyoonekana katika miji ya India na Iran, huzaliana katika vyanzo vya maji mijini - na ni sugu kwa dawa nyingi za wadudu zinazotumika kawaida.

Mbu huyo tayari amesababisha visa vya ugonjwa huo kuongezeka nchini Djibouti na Ethiopia, na hivyo kutatiza juhudi za kutokomeza ugonjwa huo.

Watafiti wanasema iwapo atasambaa kwa wingi barani Afrika anaweza kuwaweka karibu watu milioni 130 hatarini.

Chanzo: BBC