Mamlaka ya uangalizi wa wanyama pori nchini Uganda imemkamata raia wa DRC Mbaya Kabongo Bob wilayani Kisoro karibu ya mpaka wa Uganda magharibi mwa Uganda akisafirisha Kasuku wa kijivu 122 kutoka DRC kupitia Uganda.
Raia huyo wa DRC alikamatwa katika operesheni ya askari wa wanyama pori nchini Uganda UWA wakishirikiana na jeshi la UPDF na polisi kwenye mji wa mpakani wa Bunagana wilayani Kisoro.
Kwa mujibu wa msemaji wa Mamlaka ya Wanyama Pori nchini Uganda Bashir Hangi aliyezungumuza na BBC kwa njia ya simu, kukamatwa kwake ni baada ya kupata taarifa za kiintelejensia kuwa mbaya anasafirisha Kasuku hao kutoka Kishansa Congo kupitia Uganda.
Walimukuta na makasha 2 ya kasuku 122 baada ya kuwakagua wamekuta watatu wamefariki na Kasuku 119 wamehifadhiwa na Mamlaka ya wanyama pori katika bustani ya wanyama mjini Entebbe, huku wakiendelea kufanya upelelezi kujua alikokuwa anawapeleka na watu waliokuwa wakifanya bishara hiyo kupitia Uganda na baadaye anatarajiwa kufikishwa mahakamani.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya wanyama pori (UWA), Barani Afrika Kasuku wa kijivu ni wachache sana ni karibu 40,000 mpaka 100,000.
Nchini Uganda wanatarajia kuwa na idadi ya asilimia10% kati ya idadi hiyo kwa kipindi cha miaka 10 ijayo.