Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbaroni kwa kumzaba kibao Mbunge kanisani

Church Mbunge Kibao Mbaroni kwa kumzaba kibao Mbunge kanisani

Wed, 29 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanaume mmoja amekamatwa magharibi mwa Uganda na kushikiliwa katika mahabusu ya polisi baada ya kumzaba makofi mbunge katika kanisa moja Jumapili, vimeripoti vyombo vya habari nchini humo.

Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 39 alimvamia Waziri wa uchukuziambaye pia ni mbunge, Musa Ecweru alipokuwa akitoa hotuba kwa kusanyiko la waumini katika kanisa la kikatoliki la Mtakatifu Michael (St Michael Catholic Church) mjini Amuria.

"Hakujibu bali alimtazama tu. Wakristo na mapadre walishtuka,", chanzo kimoja ambacho hakikutajwa jina kililiambia gazeti linalomilikiwa na serikali nchini humo la New Vision

Walinzi wa Ecweru hatimaye walimzidi nguvu mwanaume huyo, wakamkamata na kumkabidhi kwa polisi, zilisema ripoti za vyombo vya habari.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live