Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mazungumzo ya kisiasa nchini Kenya yatarajiwa kurejelewa

Kenya Mazungumzo Mazungumzo Mazungumzo ya kisiasa nchini Kenya yatarajiwa kurejelewa

Wed, 9 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mazungumzo kati ya chama tawala cha Kenya Kwanza na muungano wa upinzani Azimio la Umoja ili kumaliza mivutano ya kisiasa kuhusu kupanda kwa gharama ya maisha na mageuzi ya uchaguzi yanatarajiwa kurejelewa.

Azimio kiliongoza maandamano makubwa mwezi Machi na Julai dhidi ya serikali ya Rais William Ruto kutaka kuundwa upya kwa tume ya uchaguzi na kupunguzwa kwa gharama ya maisha.

Hali ilizidi kuwa mbaya baada ya serikali kuanzisha ushuru wa juu mnamo Julai ili kupata mapato ya bajeti ya kwanza ya Rais Ruto.

Kundi la kutetea haki za binadamu limesema kuwa takriban watu 30 walifariki katika maandamano hayo lakini upinzani uliongeza idadi ya vifo kuwa 50.

Hakuna muda uliotolewa juu ya mazungumzo na jopo la wanachama 10 na mgawanyiko unaendelea juu ya ajenda. Timu ya kiongozi wa upinzani Raila Odinga inataka kujadili gharama ya maisha na mageuzi ya uchaguzi baada ya kushindwa katika uchaguzi mwaka jana, lakini serikali inasisitiza kuwa tayari inafanya kazi kurekebisha mfumuko wa bei na kupunguza gharama ya bidhaa za kimsingi.

Upinzani ulisimamisha maandamano mwezi Aprili na Mei ili kuruhusu mchakato sawa wa mazungumzo ya pande mbili, lakini maandamano yalianza tena baada ya mazungumzo kuvunjika. Bw Ruto na Bw Odinga wamesema kuwa mazungumzo hayo hayataleta makubaliano yoyote ya kugawana mamlaka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live