Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mazungumzo ya amani ya Sudan Kusini yafanyika Nairobi Kenya

Iuuuk.jpeg Mazungumzo ya amani ya Sudan Kusini yafanyika Nairobi Kenya

Sat, 11 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mazungumzo ya ngazi za juu kuhusu amani nchini Sudan Kusini yameanza katika jiji la Nairobi mji mkuu wa Kenya, huku miito ikitolewa na marais wa Afrika ya kumalizwa mzozo uliodidimiza uchumi wa taifa hilo kwa miaka kadhaa sasa.

Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini pamoja na kumshukuru mwenyeji wa mazungumzo hayo Rais William Ruto wa Kenya ameahidi kwamba serikali yake itafanya mazungumzo hayo kwa nia njema na kwa uwazi. Mazungumzo hayo yamefunguliwa siku ya Alkhamisi.

"Makundi ya upinzani yana nia sawa na hamu ya amani nchini Sudan Kusini ambayo baada ya kupatikana kikamilifu, italeta utulivu wa wakati wote na maendeleo ya kiuchumi katika eneo hilo, na sio tu Sudan Kusini," alisema Rais Kiir.

Kwa upande wake kiongozi wa kundi la waasi la Real-SPLM Pagan Amum Okiech amesema, "Tunahitaji kuacha mawazo ya mizozo, tunatakiwa kuacha kujiona maadui. Sisi ni ndugu, Rais Kiir, sisi ni ndugu na jamaa,".

Mazungumzo hayo yanayokutanisha makundi ya waasi na serikali, si sehemu ya makubaliano ya mwaka 2018 yaliyohitimisha vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka mitano na kusababisha vifo vya watu 40,000.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live