Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mazungumzo ya Sudan: Saudi Arabia yatarajia kusitisha mapigano

Pande Zinazozozana Sudan Zajiandaa Kwa Mazungumzo Saudi Arabia Mazungumzo ya Sudan: Saudi Arabia yatarajia kusitisha mapigano

Mon, 8 May 2023 Chanzo: Bbc

Saudi Arabia inasema inatarajia mazungumzo yaliyoanza mjini Jeddah siku ya Jumamosi kati ya makundi ya kijeshi ya Sudan yanayozozana yatafikia usitishaji wa kudumu wa mapigano.

Katika uthibitisho wa kwanza kwamba mikutano hiyo imeanza, wizara ya mambo ya nje ya Saudia ilisema pande zote mbili zinatambua haja ya kupunguza mateso ya watu wa Sudan.

Ilisema, pamoja na kusitisha mapigano, lengo lilikuwa kuhakikisha usambazaji wa vifaa vya msaada na kurejeshwa kwa huduma muhimu.

Hakujawa na maoni yoyote yaliyotolewa naeshi la Sudan au wapinzani wake wa kijeshi kuhusu mazungumzo hayo.

Mkutano wa Jeddah ni wa kwanza tangu mapigano yazuke zaidi ya wiki tatu zilizopita.

Chanzo: Bbc