Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mazungumzo ya Somalia na Somaliland iliyojitenga yanaendelea Djibouti

Somalia Somaliland Mazungumzo ya Somalia na Somaliland iliyojitenga yanaendelea Djibouti

Sat, 30 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Viongozi wa Somalia na eneo la Somaliland lililojitenga na Somalia na ambalo halitambuliwi kimataifa wamekutana nchini Djibouti ili kuanza tena mazungumzo ya kutatua mzozo ulioibuka 1991 baada ya Somaliland kujitangazia uhuru.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Taifa la Somalia (SONNA) ujumbe wa Somalia katika mazungumzo hayo unaongozwa na Rais Hassan Sheikh Mohamud na unajumuisha Waziri wa Mambo ya Ndani Ahmed Ma'alin Fiqi, Waziri wa Biashara Jibril Abdirashid na Abdikarim Hussein Guled, mjumbe maalum wa mazungumzo hayo na ujumbe wa eneo la Somaliland ukiongozwa na Rais Muse Bihi Abdi. Mazungumzo hayo ambayo yalianza Alhamisi yanatazamiwa kuendelea kwa siku kadhaa.

Mazungumzo hayo yanayosimamiwa na serikali ya Djibouti yatahusu masuala ya usalama na uchumi na hali ya kisiasa ya Somaliland. Vyombo vya habari vimeinukulu taarifa ya Ofisi ya Rais wa Somalia iliyosema kuwa duru hii ya mazungumzo inalenga "kurudisha hali ya kuaminiana" na "kukuza uhusiano wa kindugu" kati ya Somalia na Somaliland. Mazungumzo hayo yamekuja baada ya eneo la SSC-Khatumo la Somaliland kutangaza kuwa linafadhilisha kutawaliwa na serikali ya shirikisho yenye makao yake Mogadishu.

Somalia iliporomoka kama taifa moja mwaka 1991 baada ya kuondolewa madarakani Rais Siad Barre. Jamii ya kimataifa inatambua serikali ya shirikisho yenye makao yake makuu mjini Mogadishu kama mamlaka pekee halali nchini Somalia. Mbali na Somalialand kujitangazia uhuru, eneo la Puntland nchini Somalia nalo limejitangazia mamlaka ya ndani.

Somaliland ni eneo ambalo zamani lilikuwa koloni la Uingereza wakati maeneo mengine ya Somalia yalikoloniwa na Italia. Pande hizo mbili ziliungana mwaka 1960 baada ya kujinyakulia uhuru kutoka wakoloni hao wa Ulaya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live