Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mazungumzo ya Cairo kuhusu Bwawa la Renaissance yagonga ukuta

Renaissance Bwawa Cairo Mazungumzo ya Cairo kuhusu Bwawa la Renaissance yagonga ukuta

Tue, 29 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mazungumzo ya Mawaziri wa Rasilimali za Maji wa Misri, Sudan na Ethiopia kuhusu kujazwa maji na kuanza kutumika sehenu nyingine ya Bwawa la Renaissance yamemalizika bila mafanikio.

Duru mpya ya mazungumzo kuhusu Bwawa la Renaissance ilianza tena Jumapili huko Cairo nchini Misri baada ya kusimama kwa miaka miwili, ikiwashirikisha wajumbe wa nchi tatu za Sudan, Ethiopia na mwenyeji Misri.

Mohammed Ghanem, msemaji wa Wizara ya Rasilimali za Maji na Umwagiliaji ya Misri, amesema: "Hakuna mabadiliko yanayoshuhudiwa katika misimamo ya Ethiopia kuhusu Bwawa la Renaissance."

Kwa mujibu wa afisa huyo wa Misri, katika mkutano wa Cairo, Misri ilitoa mapendekezo kuhusu ujazaji wa maji na kuanza kazi Bwawa la Renaissance, lakini Ethiopia imetoa majibu hasi.

Bwawa la Renaissance (al-Nahdha) ambalo limejengwa kwenye Mto Nile umbali wa kilomita 15 kutoka mpaka wa Ethiopia na Sudan, litakuwa mtambo mkubwa zaidi wa kufua umeme barani Afrika na bwawa la saba kwa ukubwa duniani, na Cairo inasema kujazwa maji kikamilifu katika bwawa hilo ni tishio kubwa kwa maisha ya watu wa Misri.

Ujenzi wa bwawa hilo juu ya maji ya Mto Nile umesababisha migogoro mkubwa kati ya Ethiopia, Misri na Sudan, na nchi hizi mbili za Kiarabu zinasisitiza haja ya kutiwa saini makubaliano ya kulinda sehemu yao katika maji mto huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live