Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mazungumzo kuhusu bwawa la mto Nile yaanza tena

Mazungumzo Kuhusu Bwawa La Mto Nile Yaanza Tena.jpeg Mazungumzo kuhusu bwawa la mto Nile yaanza tena

Sun, 27 Aug 2023 Chanzo: Bbc

Mazungumzo kuhusu bwawa lenye utata linaloendelea Ethiopia kuhusu mto Nile yameanza tena Jumapili katika mji mkuu wa Misri Cairo.

Taarifa ya ofisi ya mawasiliano ya Ethiopia imethibitisha kuanzishwa kwa mazungumzo hayo.

Bwawa la kuzalisha umeme lenye thamani ya dola bilioni 5 limekuwa kitovu cha mzozo wa kidiplomasia kwa zaidi ya muongo mmoja kati ya Ethiopia na nchi mbili za chini ya mto Misri na Sudan ambazo zinahofia kwamba usambazaji wao muhimu wa maji uko kwenye tishio.

Mazungumzo kadhaa yalikuwa yamefanyika lakini majaribio ya kuweka wino makubaliano hayo hayajatimia. Mwezi Julai viongozi wa Ethiopia na Misri walikutana ambapo walikubali kurejea kwenye mazungumzo.

Ethiopia inasema bwawa hilo ni sehemu ya juhudi zake za kusambaza umeme kwa mamilioni ya kaya hasa katika maeneo ya mashambani.

Chanzo: Bbc