Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mazishi ya TB Joshua Kuanza Leo

T.B Joshua SCOAN?fit=700%2C394&ssl=1 Mazishi ya TB Joshua Kuanza Leo

Tue, 6 Jul 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Tukio la kuwasha mishumaa linalotarajiwa kufanyika leo (Jumatatu) litaanzisha rasmi utararibu wa mazishi ya aliyekuwa muhubiri mashuhuri wa Nigeria na muasisi wa kanisa la Synagogue Church of All Nations (SCOAN) aliyefariki mwezi uliopita, Mchungaji TB Joshua.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kanisa lake imesema, tukio hilo linatarajiwa kuanza saa kumi na mbili na nusu jioni kwa saa za Nigeria. Tukio hilo litapeperushwa laivu kwenye Televisheni ya kanisa hilo.

Kulingana na taarifa hiyo Kanisa hilo limewataka watu kubeba mishumaa kama ishara ya kuungana katika mpango wa ‘’kumheshimu’’ mtumishi wa Mungu – TB Joshua.”

Mwili wa mchungaji huyo unatarajiwa kuzikwa kwa faragha Ijumaa, Julai 11, 2021.

CC: @manyota_rich @hotpot_tz

Share this:TweetWhatsApp Related

Chanzo: globalpublishers.co.tz