Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mawaziri wapigwa marufuku kuondoka DRC

Tshisekedi Na Fayulu Kupambana Tena Uchaguzi Wa Rais Wa DRC Mawaziri wapigwa marufuku kuondoka DRC

Tue, 30 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mawaziri wawili kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, akiwemo wa Fedha, na waziri wa zamani walipigwa marufuku wikiendi hii kuondoka nchini DRC na mahakama inayochunguza tuhuma za ubadhirifu wa fedha za umma.

Katika barua ya Jumamosi, iliyorushwa Jumapili kwenye mitandao ya kijamii na kusambazwa na vyombo vya habari vya serikali, Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika Juu, Firmin Mvonde, anawataka mafisa wa Kurugenzi Kuu ya Uhamiaji (DGM) kuwapiga marufuku watu hao watatu "kuondoka Kinshasa" na "kwenye ardhi ya Kongo".

Hawa ni Mawaziri wa Fedha na Maendeleo ya Vijijini, Nicolas Kazadi na François Rubota mtawalia, pamoja na Waziri wa zamani wa Maendeleo ya Vijijini, Guy Mikulu. Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na Nicolas Kazadi, alipigwa marufuku siku ya Jumamosi kuondoka Kinshasa kuelekea Ufaransa, ambako Rais wa DRC, Félix Tshisekedi, yuko katika ziara rasmi Jumatatu na Jumanne.

Katika barua nyingine iliyotumwa kwenye mitandao ya kijamii siku ya Jumapili, ambayo uhalisi wake haukuweza kuthibitishwa mara moja, Bw. Kazadi mwenyewe alimtaka Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mvonde kuchunguza tuhuma za kutoa bili ya fedha kupita kiasi katika mkataba wa uchimbaji visima na vituo vya kusafisha maji nchini kote. Anapendekeza uchunguzi ule ule katika kesi nyingine ya madai ya bili ya pesa kupita kiasi, kuhusu uwekaji taa za barabarani mjini Kinshasa.

Kulingana na shirika la habari la AFP, Bw. Kazadi hakuweza kupatikana ili kutoa maoni yake siku ya Jumapili. Lakini alihojiwa kuhusu faili hizi mbili wakati wa mkutano uliofanyika Aprili 24 pamoja na msemaji wa serikali, uliojikita katika majadiliano ya DRC na taasisi za fedha za kimataifa.

Alikanusha ukiukwaji wowote, akidai kinyume chake aliomba pande zinazohusika katika mikataba hii kupunguza gharama zao. "Ikiwa kuna watu waliotoza pesa za kupita kiasi, hakika sio mimi," alisema juu ya uchimbaji visima, na kusema ana "huzuni" kwa kuhusishwa na uvumi huo. "Je, hii inafanywa kwa kunipaka matope? Je, ni kwa nia njema? Sijui," aliongeza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live