Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mawakili wa Uhuru na Raila watokwa na kijasho mahakamani

Ca0d45d18dc2055a Mawakili wa Uhuru na Raila watokwa na kijasho mahakamani

Wed, 30 Jun 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Makamanda wa BBI wameingia Mahakama ya Rufaa kuitetea ili isitupwe kwneye jaa na majajiMawakili Orengo na Atiende ndio wanaongoza mashambulizi upande wa Raila na Uhuru kuwasilisha utetezi dhidi ya mswada huoAliyekuwa mwanasheria mkuu pia Githu Muigai, alikuwa mbele ya majaji kutetea BBI akisema kosa lilifanyika katika Mahakama ya RufaaUamuzi wa mahakama hiyo unasubiriwa pakubwa na mirengo ya kisiasa ya handiesheki na TangatangaMawakili wa Rais Uhuru Kenyatta na kinara wa ODM Raila Odinga wanajikakamua kuokoa mswada wa BBI.

Mwanasheria mkuu Kihara Kariuki, kupitia kikosi cha mawakili waliobobea, aliitaka mahakama ya Rufaa kubadili uamuzi wa Mahakama ya Juu.

Kariuki aliambia majaji wa Rufaa kuwa kilichofanywa na Mahakama ya Juu ni shambulizi kwa Rais Uhuru Kenyatta ambapo majaji walitoa uamuzi usiofaa.

Mawakili walifanya bidii kushawishi mahakama hiyo kubatilisha uamuzi uliotolewa ili kuruhusu Wakenya kuamua kuhusu BBI kupitia refarenda.

Ken Ogeto, akiwasilisha mbele ya mahakama, alisema majaji wa Mahakama ya Rufaa walipotoshwa kuhusu waliokuwa wakiongoza mabadiliko ya kikatiba.

Aliitaka mahakama hiyo kurekebisha uamuzi uliotolewa akisema itakuwa kusahihisha makosa ya Mahakama ya Juu.

Wakati wa kutoa uamuzi wao, majaji wa mahakama ya Juu walisema ni kinyume cha sheria kwa Rais Uhuru kuongoza mswada wa mabadiliko ya kikatiba.



Aliyekuwa mwanasheria mkuu pia Githu Muigai, alikuwa mbele ya majaji kutetea BBI akisema kosa lilifanyika katika Mahakama ya Rufaa.

Alisema iwapo Wakenya hawatakubaliwa kuendelea na mchakato wa katiba, huenda wakahisi hawana namna ili kuitema katiba.

"Hilo ni hatari kwa nchi, wananchi wanaweza kufikiria njia ya pekee sasa ni kuiondoa katiba," alisema Githua wakati.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 073248269.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke