Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mawakili kesi ya raia wa Nigeria, Watanzania watulizwa Kisutu

Cc128624809882b7bc750460ab0c0169 Mawakili kesi ya raia wa Nigeria, Watanzania watulizwa Kisutu

Fri, 24 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaeleza mawakili wa washitakiwa wa kesi ya kusafi risha dawa za kulevya aina ya heroini.

Mahakama hiyo imesema waendelee kuwa na subira kwani shughuli za mahakama zitarejea katika mfumo wa kawaida hivi karibuni na hivyo watapata muda wa kuonana na wateja wao.

Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi aliwaeleza mawakili hao jana wakati kesi hiyo ilipopelekwa kwa ajili ya kutajwa. Mawakili hao wakiongozwa na wakili wa utetezi, Jeremiah Mtobesya aliomba wawe wanapata muda wa kuonana na wateja wao ambao hawakupata nafasi ya kuonana nao tangu walipopelekwa mahabusu miezi miwili iliyopita.

Washtakiwa katika kesi hiyo ni raia wa Nigeria, David Chukwu, Watanzania Isso Lupembe, mkazi wa Mbezi Luis na Allistair Mbele ambao wanakabiliwa na mashtaka ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroini kilo 268.5 na kutakatidha fedha zaidi ya Sh milioni 17. Katika hatua nyingine, wakili wa utetezi, Jeremiah Mtobsya alilalamikia kuchelewa kwa upelelezi wa shauri hilo.

Alidai, miezi miwili imeshapita tangu washitakiwa wawe mahabusu, hivyo ameiomba mahakama iamuru upande wa mashitaka kuharakisha upelelezi ili haki za washitakiwa zipatikane haraka.

Akijibu hoja hiyo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon aliahidi kushughulikia suala hilo na kueleza kwamba dawa walizokamatwa nazo washitakiwa ni nyingi na pia upelelezi unahusisha nje ya Tanzania.

Hakimu aliahirisha shauri hilo hadi Julai 14 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa. Katika kesi hiyo washitakiwa hao wanadaiwa kuwa Aprili 15 mwaka huu eneo la Mbezi Kibanda cha Mkaa, Wilaya ya Ubungo, Dar es Salaam, wote walikutwa wakisafirisha kilo 268.50 za dawa za kulevya aina ya heroini.

Mashtaka ya pili ya utakatishahi fedha ambayo wanadaiwa kulitenda kati ya Januari mosi mwaka 2016 hadi Aprili 15 mwaka huu katika maeneo tofauti jijini Dar es Salaam.

Ilidaiwa kuwa katika kipindi hicho, washitakiwa hao walitakatisha Dola za Marekani 61,500 na Sh 17,835,000 huku wakijua fedha hizo ni zao la kosa la usafirishaji wa dawa za kulevya.

Chanzo: habarileo.co.tz