Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mauzo ya mchele Sudan Kusini yaongezeka

5014dab6d3be40de72f26d56a898c700 Mauzo ya mchele Sudan Kusini yaongezeka

Tue, 1 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

UGANDA imeuza mchele kwa wingi kwa asilimia 68 nchini Sudan Kusini kuliko katika nchi nyingine za Afrika Mashariki kati ya Aprili na Juni, mwaka huu.

Ripoti ya biashara kwa nchi za Afrika Mashariki ya robo ya pili ya mwaka huu inaeleza kuwa, kwa kipindi hicho Uganda ilisafirisha tani 31,411 za mchele nchini humo, huku Tanzania ikisafirisha asilimia 21 na Somalia asilimia 11.

Mwaka 2018, serikali ya Uganda ilizuia uingizaji wa mchele ili kulinda wakulima wa ndani.

Mahitaji ya mchele Uganda kwa siku ni tani 7,158 na kwa kipindi hicho nchi hiyo ilisafirisha bidhaa nyingine za chakula pamoja na maharage.

Ripoti hiyo ilisema Uganda ilisafirisha tani 18,098 za maharage makavu nchini Sudan Kusini, huku Kenya ikisafirisha tani 11,136.

Takwimu za Benki ya Uganda zinaonesha, katika kipindi cha miaka 25 kuanzia mwaka 1994, kiwango cha uzalishaji maharage kimekuwa kikiongezeka kwa wastani wa asilimia 8.5 kutoka dola za Marekani milioni 12.64 kwa tani 37,000 zilizouzwa mwaka 1994 hadi dola milioni 99.6 kwa tani 218,000 mwaka 2018.

Ripoti ya Ukanda wa Afrika Mashariki inaeleza kuwa, katika ukanda huo, uzalishaji wa mchele mwaka huu unatarajiwa kuongezeka.

Chanzo: habarileo.co.tz