Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mauzo ya kahawa nje yaongezeka mara dufu

6abaacd147b3a4cf40bd224908a14521 Mauzo ya kahawa nje yaongezeka mara dufu

Tue, 13 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MAUZO ya kahawa katika soko la China kupitia kampuni kongwe ya biashara ya mtandaoni ya Alibaba yameongezeka kwa kiasi kikubwa katika kipindi cha mwaka jana.

Kwa mujibu wa taarifa ya kampuni hiyo, biashara ya kahawa kwa njia ya mtandao imepanda kwa asilimia 400 ikilinganishwa na vipindi vya miaka ya 2018 na 2019 ambapo biashara hiyo pia ilifanyika kwa njia ya mtandao.

Tangu mwaka 2018, Rwanda imekuwa ikiuza aina mbalimbali ya bidha za kahawa hususan katika kampuni zinazojishughulisha na soko la mtandaoni kama vile Tmall Global ambayo ni mshirika mmkubwa wa Alibaba.

Mafanikio hayo yamewezeshwa kwa kiwango kikubwa na mtandao mzuri wa Jukwaa la Biashara la Dunia (EWTP) ambalo Rwanda ilijiunga nalo mwaka 2018 kwa kusaini makubaliano na kampuni ya biashara mtandaoni.

Kupanda kwa mauzo ya kahawa ya Rwanda nchini China kumesaidia kwa kiwango kikubwa kutangazwa na kuwa maarufu kwa mauzo ya nje miongoni mwa watumiaji na wadau wengine kutoka China.

Kampuni ya Rwanda inayomilikiwa na wakulima wa kahawa imesema kuwa, katika kipindi cha kuanzia mwaka jana hadi Januari mwaka huu, imefanikiwa kuuza tani 7.2 za kahawa kwa kampuni mbalimbali za China.

Chanzo: www.habarileo.co.tz