Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mauritius imebatilisha sheria iliyoharamisha mahusiano ya watu wa jinsia moja

Mauritius Imebatilisha Sheria Iliyoharamisha Mahusiano Ya Watu Wa Jinsia Moja Mauritius imebatilisha sheria iliyoharamisha mahusiano ya watu wa jinsia moja

Thu, 5 Oct 2023 Chanzo: Bbc

Mauritius imebatilisha sheria ya enzi za ukoloni iliyoharamisha mahusiano ya watu wa jinsia moja.

Siku ya Jumatano, Mahakama ya Juu ya nchi hiyo ilitangaza kuwa Kifungu cha 250 cha Sheria ya Jinai ya Mauritius, ambacho kilianza mwaka 1898, kilikuwa kinyume cha katiba.

Chini ya sheria hiyo, watu waliopatikana na hatia ya kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja walikuwa katika hatari ya kufungwa jela hadi miaka mitano.

Katika uamuzi wake, Mahakama ya Juu Zaidi ilisema kwamba sheria iliyofutwa "haikuakisi maadili yoyote ya asili ya Mauritius bali ilirithiwa kama sehemu ya historia ya ukoloni wetu kutoka Uingereza"

Uamuzi wa kufuta sheria ya kupinga mapenzi ya jinsia moja unarudi nyuma hadi Oktoba 2019, wakati vijana wanne wa Mauritius kutoka kundi la haki za Young Queer Alliance waliwasilisha pingamizi la kisheria dhidi ya sheria ya mapenzi ya jinsia moja kwa "kukiuka haki zao za kimsingi na uhuru".

Umoja wa Mataifa na mashirika kadhaa ya kutetea haki za binadamu yamepongeza uamuzi huo.

"Umoja wa Mataifa umefurahishwa na uamuzi wa Mauritius kujiunga na orodha inayokua ya nchi za Kiafrika zinazolinda haki za binadamu za kila mtu, ikiwa ni pamoja na watu wa LGBTQI+," UNAIDS ilisema katika taarifa.

Kwa uamuzi huo, Mauritius inajiunga na orodha inayokua ya nchi za Afrika ambazo zimehalalisha mapenzi ya jinsia moja, ikiwa ni pamoja na Angola, Botswana, Seychelles na Msumbiji.

Chanzo: Bbc