Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mauaji ya kikabila yalifanyika Darfur, Uingereza yasema

Mauaji Ya Kikabila Yalifanyika Darfur, Uingereza Yasema Mauaji ya kikabila yalifanyika Darfur, Uingereza yasema

Wed, 18 Oct 2023 Chanzo: Voa

BBC imeona ushahidi mpya wa mauaji ya kikabila ambazo zimekumba Sudan Magharibi tangu mapigano yazuke kati ya makundi mawili hasimu ya kijeshi mwezi Aprili.

Uchambuzi wa data za satelaiti na mitandao ya kijamii unaonyesha takriban vijiji 68 huko Darfur vimechomwa moto na wanamgambo wenye silaha tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe kuanza.

Waziri wa Uingereza wa Afrika, Andrew Mitchell, aliiambia BBC kuwa hii ina "ishara zote mauaji ya kikabila". Ni mara ya kwanza kwa serikali ya Uingereza kutumia neno hilo kuelezea kinachoendelea nchini Sudan.

Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, ambaye anaongoza upande mmoja katika mzozo huo - Jeshi la Sudan (SAF) - aliiambia BBC kuwa atashirikiana na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kuwafikisha walio na hatia mbele ya sheria.

Mengi ya mauaji ya kikabila zinalaumiwa kwa wanamgambo ambao ni sehemu ya - au washirika wa - Rapid Support Forces (RSF), kikundi cha kijeshi kinachopigana na SAF kwa udhibiti wa nchi.

RSF imekanusha mara kwa mara kuhusika na ghasia katika eneo hilo na imetaka uchunguzi huru wa kimataifa.

Uchambuzi huo umefanywa na Kituo cha Ustahimilivu wa Taarifa, chombo cha utafiti ambacho kwa sehemu kinafadhiliwa na serikali ya Uingereza, ambacho kinakusanya ushahidi wa wazi kuhusu mapigano nchini Sudan.

Wanatumia teknolojia ya NASA ya kutambua moto. Wanatazama picha za satelaiti ili kugundua moshi na majengo yaliyoteketea. Zinalinganisha hayo yote na picha kutoka ardhini kwenye mitandao ya kijamii, ambazo zimepangwa kwa kutumia ramani na picha.

Mioto ya hivi punde iliyothibitishwa ilikuwa katika kijiji kiitwacho Amarjadeed, kusini mwa Darfur, ambapo picha za NASA na satelaiti zilionyesha makovu ya moto kati ya 18 Septemba na 9 Oktoba.

Hivi ndivyo Kituo cha Ustahimilivu wa Taarifa kilianzisha jinsi msafara mmoja wa wanamgambo ulichoma moto kwa takriban vijiji tisa kwa siku moja, 16 Agosti.

Chanzo: Voa