Steven Yamba (44) mfanyabiashara wa nchini Zambia ameripotiwa kumshushia kipigo kikali mke wake wa ndoa Kangwa Mwango (33) na kufariki dunia juzi Desemba 25, 2021 siku ya Christmas, majira ya saa 3, asubuhi.
Imeelezwa kuwa, baada ya kuona hali ni mbaya, alijaribu kumnyanyua mkewe ili ampeleka hosptali, lakini alipogundua tayari ameshafariki na yeye akaamua kukimbilia dukani na kununua dawa ya kuulia wadudu, ambayo alikunywa na kufariki dunia papo hapo.
Jeshi la Polisi nchini humo wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kumesema uchunguzi wa awali umeonesha kuwa majira ya saa 1 usiku, katika mkesha Christmas, mfanyabiashara huyo alianza kumpiga mkewe hadi asubuhi, na kuvuja kwa damu nyingi na kupata majeraha mbalimbali sehemu za mwili wake hali iliyosababisha umauti huo.
Polisi bado wanaendelea na uchunguzi zaidi kutokana na tukio hilo lililowaacha watu midomo wazi, huku chanzo cha mwanaume huyo kutekeleza unyama huo kwa mkewe kikiwa hakijawekwa wazi badi.