Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mauaji Cameroon: Watu saba wauawa wengine watekwa

Mauaji Came Mauaji Cameroon: Watu saba wauawa wengine watekwa

Mon, 27 Jun 2022 Chanzo: VOA

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesema Jumatatu kwamba waasi wanaotumia lugha ya kiingereza nchini Cameroon wameua takriba watu 7 pamoja na kuteka nyara watu kadhaa tangu mwanzoni mwa mwaka huu.

Ghasia zimekuwa zikishuhudiwa kaskazini magharibi na kusini magharibi mwa Cameroon kwa karibu miaka mitano wakati serikali ikikabiliana na waasi wanaotumia lugha ya kiingereza wanaotaka kujitenga na wale wanaotumia lugha ya kifaransa, na ambao ni wengi nchini humo.

Waasi hao wamekuwa wakilenga shule pamoja na kushambulia angalau chuo kimoja kikuu. Ripoti ya Human Rights Watch ni kutokana na mahojiano kutoka kwa watu walioathiriwa, mashuhuda, rekodi za kimatibabu pamoja na ushahidi wa kujionea.

Tangu mwaka wa 2017, eneo linalotumia lugha ya kiingereza limedai kutengwa na kwa hivyo kuitisha uhuru wao wa eneo wanaloita Ambazonia. Rais wa Cameroon Paul Biya mwenye umri wa miaka 89 ameongoza taifahilo kwa karibu miaka40, wakati akiamuru misako mikali dhidi ya waasi.

Chanzo: VOA