Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Matungu: ODM Yaelekea Mahakamani Kupinga Ushindi wa Peter Nabulindo wa ANC

3ea874d4322ed874 Matungu: ODM Yaelekea Mahakamani Kupinga Ushindi wa Peter Nabulindo wa ANC

Tue, 30 Mar 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Chama cha ODM kimedai kwamba uchaguzi mdogo wa Matungu ulikumbwa na wizi wa kura na kimetaka ufutiliwe mbali

- Mgombea wa ODM David Were aliibuka wa pili huku mpinzani wake Peter Nabulindo akiibuka mshindi kwa kura 14, 257

- Chama cha ANC kimekashifu hatua ya chama cha ODM kwenda mahakamani kupinga matokeo hayo kikidai kwamba vyama hivyo viwili vipo chini ya Muungano wa NASA

Chama cha ODM kimedai kwamba uchaguzi mdogo uliofanyika eneo bunge la Matungu ulikumbwa na dosari nyingi ikiwemo ubadhirifu, ghasia miongoni mwa makosa mengine.

Katika uchaguzi huo, Peter Nabulindo wa chama cha ANC aliibuka mshindi kwa kujizolea kura 14,257 huku akifuatwa kwa karibu na David Were wa chama cha ODM.

Imebainika kwamba Were ameenda kortini kupinga matokea hayo akidai hayakuwa sahihi na ametaka yafutiliwe mbali.

Hata Hivyo, viongozi wa chama cha ANC wamekosoa hatua hiyo wakisisitiza kwamba ODM inaonyesha picha mbaya ikizingatiwa kwamba vyama vyote bado vipo chini ya muungano wa NASA.

Aidha, katibu mkuu wa ODM Edwin Sifuna amethibitisha madai hayo akisema kwamba Were ameenda kibinafsi mahakamani kupinga matokeo hayo na mojawapo ya sababu ya kuchukua hatua hiyo anadai ni ubadhirifu wa kura.

"David Were ameelekea mahakamani kupinga uchaguzi wa Nabulindo, huu ni uamuzi wa mgombeaji na miongoni mwa sababu kuu ni ubadhirifu wa kura" Sifuna alisema.

Tukio hilo limedhibitishwa na mbunge wa Lugari Ayub Savula huku akisisitiza kwamba ODM inaonyesha picha mbaya chini ya muungano wa NASA.

"ODM wameonyesha nia ya kuelekea mahakamani licha ya vyama hivi kuwa chini ya muungano wa NASA" Alifoka Savula.

Tuko.co.ke ilibaini kwamba eneo bunge la Matungu lina jumla ya wapiga kura 62,386 na ni wapiga kura 33, 824 pekee waliojitokeza kupiga kura katika uchaguzi mdogo uliofanyika Machi 4, 2021.

Mwandani wa karibu wa naibu rais William Ruto, Alex Lanya kupitia chama cha UDA alirithika na nafasi ya tatu kwa kupata kura 5,513.

Hatua hiyo ya ODM inazidi kutia msumari kwenye kidonda huku muungano wa NASA ukizidi kuyumba yumba, hivi maajuzi kinara wa ODM Raila Odinga aliwakashifu vinara wenza katika muungano wa NASA Kalonzo, Mudavadi na Wetang'ula kwa kumtaka awaunge mkono huku akidai walimtoroka wakati aliwahitaji.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke