Mamlaka nchini Rwanda imeshtushwa na idadi kubwa ya vijana wanaojiua, huku watoto wenye umri wa miaka 11 wakiongoza kwa kujiua nchini humo. kutokana na tatizo la afya ya akili.
Wakazi wa kijiji cha Gizoni wilayani Gasabo waliamka na mshtuko mkubwa baada ya mvulana mwenye umri wa miaka 11 kujinyonga.
Baada ya kurudi nyumbani, dada zake wakubwa walikuta chumba cha kulala kikiwa kimefungwa kutoka ndani, hali iliyowafanya kuhisi kwamba huenda kuna jambo baya linaendelea.
Walilazimika kuvunja nyumba na kukuta mwili wake ukiwa unaning’inia kwenye kamba.
Wazazi wa mtoto huyo wamesema kwamba hakua na tatizo lolote , na kwamba kifo chake kimeacha amswali mengi kwenye familia hiyo.
Visa vingine vya kujiua miongoni mwa vijana wenye umri kati ya miaka 18 na 35 vinaendelea kuripotiwa kote nchini Rwanda, sababu kubwa ikitajwa kwamba ni afya ya akili.
Kwa muhibu wa ofisi ya uchunguzi ya Rwanda (RIB) kumeripotiwa visa 576 vya kujiua nchini humo kati ya mwaka 2020-2021 ikilinganishwa na kesi 291 zilizosajiliwa mwaka 2019-2020. Ndani ya mwaka huu pekee kuna visa 285 vua kujiua .