Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Matukio makubwa ya Mapinduzi barani Afrika ndani ya Mwaka 2021

Screenshot 2021 10 26 At 10.png Matukio makubwa ya Mapinduzi barani Afrika ndani ya Mwaka 2021

Tue, 26 Oct 2021 Chanzo: JamiiForums

Katika muda wa mwaka mmoja, wanajeshi wametwaa mamlaka katika nchi tatu kusini mwa jangwa la Sahara.

Wanajeshi wa kikosi maalumu walipindua serikali ya kiraia ya Mali ambapo Kanali Assim Goita alijitangaza rais.

Miezi michache baada ya Kanali Goita kuongoza mapinduzi Mali, wanajeshi walitwaa mamlaka Chad baada ya kifo cha Rais Iddris Derby.

Mwanawe Derby, Jenerali Mahamat Derby alitangazwa rais wa nchi hiyo kwa usaidizi wa Ufaransa iliyotawala nchi hiyo enzi za ukoloni.

Mapema mwezi huu Septemba, Kanali Mamady Doumbouya aliongoza wanajeshi wa kikosi maalum, kupindua serikali ya kiraia ya Guinea na kumzuilia Rais Alpha Conde.

Mapema Jumanne, serikali ya mpito ya Sudan ilitangaza kuwa ilizima jaribio la mapinduzi mwaka mmoja baada ya kuondolewa mamlakani kwa Rais Omar el Bashir.

Msururu wa mapinduzi haya unazua kumbukumbu ya hali iliyokumba nchi kadhaa za kusini mwa jangwa la Sahara miaka ya kwanza baada ya kupata uhuru.

Wimbi la mapinduzi miaka ya sitini na sabini lilisababishwa na ukosefu wa usawa, utawala wa kiimla na wanajeshi vijana waliotaka kuonja mamlaka baada ya kupata mafunzo ng’ambo.

Watawala wa kijeshi waliua na kuwazuilia wapinzani wao, walikandamiza haki za raia wao, wakapora rasilimali na matokeo yakawa ni bara la Afrika kudumaa kimaendeleo.

Chanzo: JamiiForums