Bunge la Seneti linatarajiwa kuagiza Waziri wa Elimu, Ezekiel Machogu, pamoja na wadau wengine wa Wizara ya Elimu kufika mbele ya Kamati ya Elimu kufafanua maswali yaliyoibuka miongoni mwa Wakenya baada ya matokeo ya Mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne (KCSE 2022) kutangazwa
Wakenya walihoji kilichopelekea Shule ambazo hazijawahi kurekodi Matokeo mazuri Miaka ya nyuma Mwaka huu zimefaulu kwa kiasi kikubwa na kuibua Sintofahamu kuhusu Uwepo wa Udanganyifu.
Mfano Sekondari ya Nyambaria iliyoko kaunti ya Kisii watahiniwa walikuwa ni 488. Mwanafunzi wa mwisho alipata Alama ya B kumaanisha kwa Wanafunzi wote walifaulu.