Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Matokeo ya Uchaguzi Mkuu Morroco, Upinzani wanyakua Majimbo mengi

Result Morroco Morroco yatangaza matokeo uchaguzi Mkuu, upinzani wanyakua majimbo mengi

Fri, 10 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama cha National Rally of Independents Party (RNI) cha nchini Morroco kimethibitisha kushinda nafasi nyingi za uwakilishi Bungeni katika uchaguzi mkuu wa nchini humo.

Katika nafasi zote 395 za ubunge zilikuwa zikiwaniwa, chama hicho kimenyakua nafasi 97 za uwakilishi, huku Chama cha Islamist Justice and Development (PJD) kilichoongoza kuanzia mwaka 2011 kikiwa na nafasi 12 pekee kutoka nafasi 125 kwenye uchaguzi uliopita wa mwaka 2016.

Aidha Chama cha RNI kimeahidi kutoa nafasi za kazi zaidi ya milioni moja ili kuweza kuinua uchumi uliotetereshwa na janaga la UVIKO-19, ikiwa ni pamoja na kuboresha sekta ya afya, elimu kwa kuongeza mishahara ya watumishi sambamba na kutoa mafao ya uzeeni.

Kinacho subiriwa sasa nchini humo ni Mfalme kuteuwa Waziri Mkuu ambpo kwa mujibu wa taratibu zao ni kuwa Waziri Mkuu anateuliwa kutoka katika chama kilichoshinda nafasi nyingi za uwakilishi, kisha atarusiwa kuunda serikali kwamaana ya kuunda baraza la mawaziri pamoja na kufanya uteuzi wa wakuu wa Idara na Mikoa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live