Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Matokeo ya KSCE 2020 yametangazwa, 893 wapata gredi ya A

15b44776b0891e45 Matokeo ya KSCE 2020 yametangazwa, 893 wapata gredi ya A

Mon, 10 May 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Waziri wa Elimu Prof. George Magoha ametangaza rasmi matokeo ya Mtihani wa KCSE 2020.

Mtahiniwa Simuyu Robinson Wanjala wa Shule ya Upili ya Murang'a ndiye aliyeibuka wa kwanza.

Kulingana na matokeo hayo, yaliyotangazwa Jumatatu, Mei 10, watahiniwa 893 walipata alama ya A huku 143, 140 wakipata alama zitakazowawezesha kuingia moja kwa moja katika Vyuo Vikuu.

Wakati huohuo, watahiniwa wa kike walikuwa wengi zaidi katika Kaunti 15.

Kutangazwa kwa matokeo kunatoa fursa ya udahili katika Vyuo Vikuu, Vyuo Anuwai na Taasisi za Kiufundi.

Takwimu za Knec zinaonyesha kuwa watahiniwa 752,933 walisajiliwa kufanya mtihani wa KCSE mwaka uliopita katika vituo 10,437.

Usahihishaji ulianza mara tu baada ya kumaliza mitihani mnamo Aprili 16.

Wasahihishaji wasiopungua 27,284 walifanya kazi ya kusahihisha karatasi za watahiniwa katika shule 33 za kitaifa katika maeneo manane, zamani yakiitwa mikoa.

Mengi kufuatia punde...

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke