Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Matiang'i ampiga mkwara Ruto "Hata Hitler alikuwa Hasla"

F04a1430ba3640bb Naibu Rais William Ruto na Waziri Matiang'i

Thu, 26 Aug 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang'i amekosoa vuguvugu la Naibu Rais William Ruto la 'hasla' akilitaja kama mkakati mbaya wa kupiga siasa.

Waziri Matiang'i alihoji kuwa Hitler alikuwa akiendesha kampeni ya kumaliza umaskini miongoni mwa halaiki ya watu lakini hatimaye aliwageuka.

Aliwaonya Wakenya dhidi ya kumchagua William Ruto akisema anatoa ahadi zisizokuwa za kuaminikaRuto amekuwa akipigia debe vuguvugu la 'hasla' ambalo linalenga kuinua uchumi kupitia mfumo wa bottom-up akiazimia kuwania urais mara ya kwanza

Akizungumza wakati wa mkutano na Baraza Kuu la Makanisa Jumatano, Agosti 25, jijini Nairobi, Matiang'i alidai kuwa dikteta Mjerumani Adolf Hitler pia alikuwa 'hasla'.

Matiang'i alihoji kuwa Hitler alikuwa akiendesha kampeni ya kumaliza umaskini miongoni mwa halaiki ya watu lakini hatimaye aliwageuka.

"Hitler wakati wa kampeni nchini Ujerumani aliwambia Wajerumani wamupe miaka mitano na atawabadilishia nchi hiyo. Kwa kweli alibadilisha Ujerumani kwa sababu aliwaua Wayahudi na kufanya mambo mengine mabaya zaidi," alisema.



Aliwaonya Wakenya dhidi ya kumchagua Ruto akisema anatoa ahadi zisizokuwa za kuaminika.

"Lakini alizunguka (Hitler) nchi nzima akipora mali akichuma nafuu kwa umaskini na kisha kuitumia kama silaha. Wacha tusiingie kwenye mtego kupitia vitu visivyokuwa vya kuaminika," alisema Matiang'i kama livyoripoti NTV.

Waziri huyo alisema Uchaguzi Mkuu wa 2022 utakuwa wakati wa kihistoria kwa vijana kushinikiza uongozi bora na kujiepusha na vita.

Mfumo wa uchumi wa William Ruto wa bottom-up Ruto amekuwa akipigia debe vuguvugu la 'hasla' ambalo linalenga kuinua uchumi kupitia mfumo wa bottom-up akiazimia kuwania urais mara ya kwanza.

Mwanasiasa huyo mzawa wa Sugoi, ametangaza azma yake ya kutaka kumrithi Rais Uhuru Kenyatta na amekuwa akiwavizia vijana na Wakenya wasiokuwa na kazi akisema serikali yake itakuwa ya watu maskini.

Ruto alisema wakati umefika kuwainua wanabiashara wadogo badala ya wanasiasa wenye ushawishi.

Vuguvugu la hastla limemshuhudia Ruto akishtumiwa na pia akisifiwa huku siasa za urithi za mwaka 2022 zikipamba moto.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke