Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Matatani kwa kudhalilisha fedha Nigeria

Bobrisky.jpeg Matatani kwa kudhalilisha fedha Nigeria

Thu, 4 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mmoja wa watu maarufu nchini Nigeria, mwanamke aliyebadili jinsia, aitwaye Bobrisky, amekamatwa na polisi kwa mashtaka ya kudhalilisha fedha za nchi hiyo.

Bobrisky, ambaye jina lake halisi ni Idris Okuneye, anadaiwa kudhalilisha na kuzichana noti za fedha wakati wa shughuli ya uzinduzi wa filamu jijini Lagos, mamlaka zimeliambia Shirika la Utangazaji la Uingereza.

Wamesema alizirusha noti hewani kwa mtindo uitwao “spraying” kama ishara ya kushukuru.

Mtindo huo wa ku ‘spray’ hufanywa sana nchini Nigeria katika sherehe mbalimbali na hata za harusi.

Ni kosa iwapo fedha zitadondoka sakafuni ambapo zinaweza kukanyagwa.

Bobrisky anadaiwa ku ‘spray’ noti wakati wa uzinduzi wa filamu ya Ajakaju, filamu ambayo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu, iliyochezwa na Eniola Ajao.

Video za tukio la kurusha fedha zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Bobrisky ana wafuasi zaidi ya milioni tano kwenye Instagram, imeripoti BBC.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live