Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mataifa ya Ulaya yatoa tahadhari ya mashambulizi ya kigaidi Kenya

0fgjhs1g4fohe7pt9g Mataifa ya Ulaya yatoa tahadhari ya mashambulizi ya kigaidi Kenya

Fri, 28 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ubalozi wa Ufaransa umewataka raia wake wawe makini na kujiepusha na maeneo ya umma katika siku zijazo, ikiwemo wikendiNairobi, Lamu, Garissa na maeneo yanayokaribia mpaka wa Kenya-Somalia.

Maeneo hayo yametajwa kuwa kwenye hatari zaidi na itakumbukwa kuwa Mwezi Juni 2021, Marekani iliwatahadharisha raia wake dhidi ya kuzuru Kenya kufuatia ongezeko la visa vya utekaji nyara.

Mabalozi ya Ufaransa, Uingereza, Uholanzi na Ujerumani yameonya uwezekano wa mashambulizi ya kigaid katika ardhi ya Kenya.

Kwenye taarifa iliyotolewa siku ya Alhamisi Januari 27, ubalozi wa Ufaransa uliwataka raia wake kuwa makini na kujiepusha na maeneo ya umma katika siku zijazo ikiwemo wikendi.

"Kumekuwapo na tishio la usalama mara kwa mara dhidi ya Raila wa ughaibuni wanoishi nchini Kenya. Pana hatari ya kuzuru maneo ya umma na raia wa kigeni hususan hoteli, migahawa, maeneo ya burudani, maduka makuu, maeneo ya biashara haswa jijini Nairobi," imesema taarifa hiyo

Chanzo: www.tanzaniaweb.live