Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mataifa ya Afrika kumaliza vita Ukraine, Russia?

Rais Zelensky Atembelea Mji Uliokombolewa Mataifa ya Afrika kumaliza vita Ukraine, Russia?

Fri, 16 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Viongozi wa Nchi za Afrika wakiongozwa Rais wa Afrika Kusini Cyrill Ramaphosa na Rais wa Senegal, Macky Sall.

wanautembelea Mji Mkuu wa Ukraine, Kyiv kama sehemu ya ujumbe wa amani unaolenga kuanzisha juhudi za kuumaliza uhasama kati ya Urusi na Ukraine.

Viongozi hao wa Nchi za Afrika wameanza juhudi zao za kusuluhisha ambapo watakutana na Rais wa Ukraine na kisha Rais wa Urusi Vladmir Putin kila mmoja peke yake.

Ramaphosa na Wajumbe wenzake tayari wameshawasili Ukraine kwa ajili ya mazungumzo na Rais Volodymyr Zelensky yatakayofanyika leo Ijumaa na kisha wanatarajiwa kukutana na Rais Vladimir Putin wa Urusi hapo kesho Jumamosi Mjini St Petersburg.

Viongozi hao wa Afrika watapendekeza hatua za kujenga hali ya kuaminiana ili kuleta amani hatua hizo ni pamoja na Urusi kuyarudisha Majeshi yake nyuma, kuziondoa silaha zake za nyuklia kutoka Belarus na kuiweka kando, hati ya Mahakama ya Kimataifa (ICC) ya kukamatwa kwa Rais Putin pamoja na kuondolewa kwa vikwazo vilivyowekwa kwa Urusi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live