Shirika la Afya Duniani (WHO) na washirika wake wamesema karibu dozi milioni 18 za chanjo ya kwanza ya malaria duniani itawasilishwa kwa mataifa 12 ya Afrika ifikapo 2025.
Miongoni mwao ni Malawi, Ghana na Kenya, ambapo chanjo ya Mosquirix tayari imetumika katika majaribio.
Huku mahitaji yakizidi ugavi, kipaumbele kitaenda kwa nchi zenye uhitaji mkubwa zaidi, na ambapo matokeo ya juu zaidi yatapatikana.
Msumbiji na Sudan zimetengwa kwa sababu ya viwango vyao vya juu vya kuacha chanjo.
WHO inasema chanjo hiyo - iliyotengenezwa na kampuni ya Uingereza ya GSK - inaweza kuokoa maisha ya mtu mmoja kwa kila watoto 200 wanaochanjwa.
Malaria huua takriban watoto nusu milioni wa Kiafrika chini ya miaka mitano kila mwaka.