Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maswali yaibuka kutekwa bosi kiwanda cha sukari

Bosi Pic SUKARI Maswali yaibuka kutekwa bosi kiwanda cha sukari

Mon, 28 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maswali kuhusu kutekwa kwa mwenyekiti wa kiwanda cha sukari cha Kabras Sugar Jaswant nchini Kenya, Singh Rai Ijumaa, yameibuka ikiwemo kuhusika kwa vyombo vya dola nchini humo.

Utekaji nyara huo wa umeibua maswali kuhusu iwapo nchi inarudi nyuma katika enzi vyombo vya usalama vilidaiwa kuhusika na tuhuma hizo.

Kwa mujibu wa Nation, mfanyabiashara huyo alitoweka wakati watu waliokuwa na silaha waliokuwa kwenye gari la kubebea mizigo walipozuia gari yake aina ya Toyota Land Cruiser kwenye makutano ya barabara ya Wood Avenue Kilimani, mkabala na Kenwood Apartments majira ya saa kumi jioni.

Picha zilizorekodiwa na kamera za CCTV zinaonyesha wanaume wanne wakitoka kwenye gari aina ya Toyota Pick Up na kuwavuta kwa lazima watu waliokuwa ndani ya gari la bilionea huyo kisha kuondoka nao kuelekea Barabara ya Galana huku gari yake ikitelekezwa barabarani.

Kamanda wa Polisi wa Kaunti Ndogo ya Kilimani, Moss Ndiwa aliviambia vyombo vya habari nchini humo kuwa, siku iliyofuata, binti wa Rai akiwa na wakili, walikwenda kituo cha polisi kutoa taarifa ya kupotelewa na baba yao.

"Pia alithibitisha kuwa gari lililovutwa hadi kituoni lilikuwa lake la baba yake," afisa huyo aliongeza.

Familia hiyo ilisambaza picha za CCTV za tukio hilo, jambo lililowafanya kuamini kwamba Rai alikuwa huenda ametekwa nyara.

Ndiwa alisisitiza kwamba polisi hawawezi kuthibitisha kuhusiana na tukio hilo.

Mapema jana, mmoja wa mawakili wanaowakilisha familia hiyo, Wakili Mwandamizi Kioko Kilukumi, alisema familia hiyo haikuwa na mawasiliano yoyote na Rai na kwamba hakuweza kupatikana kwa njia ya simu.

Jaswant ni mwanafamilia wa Rai, mmoja wa matajiri wakubwa nchini humo na sasa ana hisa kubwa katika sekta ya mafuta ya kula na sukari, akishikilia zaidi ya nusu ya soko la sukari nchini Kenya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live