Rais Uhuru Kenyatta ameagiza maafisa wa polisi kukaa chonjo akisema hali ni mbaya nchini kiusalama. Haijabainika hali ambayo Rais amezungumzia kwa sababu hakujakuwa na visa vikuu vya utovu wa usalama.
Amesema hilo wakati wa kikao cha usalama na kamati ya usalama kitaifa (National Security Council) Kulingana na msemaji wa Ikulu Kanze Dena, Rais alisema kuna hatari ya usalama na hivyo polisi wanafaa kuchangamka kila kona.
“Rais Kenyatta amewataka polisi kuwa macho zaidi. Rais Kenyatta ameamuru vikosi vya usalama kukaa macho Zaidi kote nchini kutokana na visa vya ukosefu wa usalama vinavyoendelea,” Kanze alisema kwenye taarifa