Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Masoko haramu ya silaha ya AK-47 yasambaa mji mkuu wa Sudan

Masoko Haramu Ya Silaha Ya AK 47 Yasambaa Mji Mkuu Wa Sudan Masoko haramu ya silaha ya AK-47 yasambaa mji mkuu wa Sudan

Sun, 20 Aug 2023 Chanzo: Bbc

Bei ya bunduki aina ya AK-47, mojawapo ya silaha za kivita zinazotambulika zaidi, imeshuka katika kipindi cha miezi michache iliyopita kwa asilimia 50 katika soko la biashara haramu katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum - ambayo sasa inagharimu karibu $830.

Mfanyabiashara wa muda mrefu wa silaha alihusisha kushuka kwa kasi kwa bei na ukweli kwamba soko la biashara haramu limejaa Kalashnikov iliyobuniwa na Urusi, baada ya Sudan kutumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe mwezi Aprili.

Mapigano kati ya jeshi na Wanajeshi wa Msaada wa Haraka (RSF) hupamba moto kila siku katika mitaa ya Khartoum na miji mingine miwili, Bahri na Omdurman - ambayo inaunda mji mkuu.

Akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina, mwanaume huyo ambaye ananunua na kuuza silaha alisema kuwa ingawa baadhi ya wasambazaji wake ni maafisa wa jeshi waliostaafu, wengi wao wanatoka katika safu ya RSF.

Ugavi ulizidi mahitaji, hasa baada ya kile wenyeji wanakitaja kama Vita vya Bahri, vilivyopiganwa katikati ya Julai, karibu miezi mitatu katika mzozo ambao umeiharibu Sudan.

Hapo awali silaha za magendo zilikuwa zikiuzwa hasa kwa waasi na wanamgambo waliohusika katika migogoro ya muda mrefu nchini Sudan, au mataifa jirani kama Chad.

Chanzo: Bbc