Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashujaa Day: Rais wa Malawi Lazarus Chakwera awasili Nairobi

D328b7d85f44986f Mashujaa Day: Rais wa Malawi Lazarus Chakwera awasili Nairobi

Tue, 19 Oct 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Rais wa Malawi Lazarus Chakwera aliwasili Kenya Jumanne kwa ziara ya siku tatu ya Serikali.

Chakwera ambaye ameandamana na Mke wake Monica Chakwera, atakuwa Mgeni wa Heshima katika sherehe za Siku ya Mashujaa ya mwaka huu ambayo itafanyika katika uwanja wa Wang’uru katika Kaunti ya Kirinyaga Jumatano.

Rais Uhuru Kenyatta atakuwa mwenyeji wa Rais huyo wa Malawi katika Ikulu, Nairobi AlhamisiIjumaa wiki iliyopita, Waziri wa Mambo ya Ndani Dkt. Karanja Kibicho aliagiza kwamba sherehe za 58 za Mashujaa Day zifanyike huko Kirinyaga pekee bila ya zingine katika kaunti zingine kwani imekuwa kawaida.

Kiongozi huyo ambaye alikuwa ameandamana na Mke wake Monica Chakwera, atakuwa Mgeni wa Heshima katika sherehe za Siku ya Mashujaa ya mwaka huu ambayo itafanyika katika uwanja wa Wang’uru katika Kaunti ya Kirinyaga Jumatano.

Rais Chakwera alipokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta na Waziri wa Ulinzi Eugene Wamalwa na mwenzake wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia (ICT) Joe Mucheru.

Rais Uhuru Kenyatta atakuwa mwenyeji wa Rais huyo wa Malawi katika Ikulu, Nairobi Alhamisi.

Mamia ya wageni wanatarajiwa kufika katika sherehe za Siku ya Mashujaa huko Kirinyaga.

Ijumaa wiki iliyopita, Waziri wa Mambo ya Ndani Dkt. Karanja Kibicho aliagiza kwamba sherehe za 58 za Mashujaa Day zifanyike huko Kirinyaga pekee na hakuna sherehe zitakazoruhusiwa katika kaunti zingine kwani imekuwa kawaida.

Hapo awali, Makamishna wa Kaunti wangeongoza sherehe kama hizo huko mashinani.
Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke