Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashujaa 6 wanaopambana na janga la corona Afrika

101497 Pic+mashujaa Mashujaa 6 wanaopambana na janga la corona Afrika

Tue, 7 Apr 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Wakati ugonjwa wa virusi vya corona Covid- 19 ukiendelea kuitesa dunia, baadhi ya watu maarufu duniani wametumia mali zao kuchangia mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

Miongoni mwao ni wanawake sita wanaofanya kazi katika kampuni nchini Libya ambao wamebadilisha kazi za kampuni hiyo kutoka kutengeneza nguo za kisasa hadi nguo wanazovaa wahudumu wa afya wanaohudumia wagonjwa.

Wanawake hao wanashona nguo za madaktari na wauguzi katika kiwanda kimoja cha nguo cha Fashion House jijini Tripoli.

Wote wamejitolea kufanya kazi hiyo huku baadhi yao wakiamua kulala kiwandani.

Hadi kufikia sasa wametengeneza nguo 50 na kwa sasa wameanza kundi jingine la nguo hizo.

Mapema wiki iliyopita, wahudumu wa afya katika jiji la Tripoli walipongeza juhudi hizo.

Pia Soma

Advertisement
“Wazo hili lilianza wakati daktari katika Hospitali ya al-Jalaa jijini Tripoli alipoomba msaada kutoka kwa wafanyabiashara mbalimbali,” alisema mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Fashion House, Najwa Taher Shokriy.

Alianzisha kampuni hii mwaka mmoja uliopita, lakini mipango ya kupanua kampuni hii ameiweka pembeni kidogo kukabiliana na janga hili lililosababisha matatizo makubwa katika sekta ya afya.

Kwa upande mwingine, kundi la wauza maua la Paarl, mji uliopo katika eneo ambalo ni kitovu cha utengenezaji wa mvinyo nchini Afrika Kusini, limeungana na kupamba jengo moja.

Wakiwa na maua 600 kutoka kampuni ya maua ya Adene, walipamba nje ya jengo la zamani la wazee la Huis Vergenoegd.

Wakazi wa jengo hilo wametakiwa kutotoka nje tangu katikati ya mwezi Machi, lakini waliruhusiwa kutoka kutazama jengo lilivyopambwa, kukiwa kunanukia harufu nzuri ya maua ya waridi, kwa mujibu wa ukurusa wa Facebook wa kampuni ya maua.

Nchini Kenya mmiliki mmoja wa nyumba amewaambia wapangaji wake 34 kwamba hawatalipa kodi ya mwezi Machi na Aprili kwasababu anaelewa kwamba janga la virusi hivyo limesababisha msukosuko wa kifedha kwa kaya nyingi.

Michael Munene anamiliki nyumba 28 magharibi mwa Kenya eneo la Nyandarua na kila mpangaji analipa Sh3,000 za Kikenya (sawa na zaidi ya Sh60,000 za Kitanzania) kila mwezi.

Pia ana majengo sita ya kibiashara ambako wapangaji hulipa Sh5,000 za Kenya kila mwezi. Ikiwa hakuna atakayelipa atapoteza zaidi ya dola 2,000 (sawa na zaidi ya Sh4.5 milioni za Kitanzania).

Munene anayepongezwa na watu mbalimbali, aliwahi kuwa mpangaji na aliwahi kufukuzwa kwa sababu ya kushindwa kulipa kodi ya mwezi.

Mcheza dansi afanya onyesho mtandaoni

Nchini Tunisia mcheza dansi ya belly, Nermine Sfar amekuwa akifanya onyesho mtandaoni kuburudisha wasiotoka nyumbani.

Chanzo: mwananchi.co.tz