Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashirika ya ndege yasitisha safari kuelekea Sudan kwenye mapigano

Mashirika Ya Ndege Yasitisha Safari Kuelekea Sudan Kwenye Mapigano Mashirika ya ndege yasitisha safari kuelekea Sudan kwenye mapigano

Sat, 15 Apr 2023 Chanzo: Bbc

Ndege zimekuwa zikigeuza na kurudi zilikotoka badala ya kutua katika uwanja wa ndege wa Khartoum, baada ya ripoti kwamba watu wawili wameuawa wakati kombora lililopiga ndege ya abiria.

Tangu wakati huo, mashirika mawili ya ndege yametoa taarifa.

Shirika la ndege la Saudi Arabian Airlines linalomilikiwa na serikali lilisema kwamba moja ya ndege zake aina ya Airbus A330 "ilipata ajali" huko Khartoum kabla ya safari yake iliyopangwa kuondoka kuelekea Riyadh saa 07:30 GMT.

Shirika hilo la ndege liliongeza kuwa linashirikiana na ubalozi wa Saudia nchini Sudan kubaini kilichotokea na kwamba safari za ndege za kwenda na kurudi Khartoum zimesitishwa kwa muda usiojulikana.

Shirika la ndege la Misri la EgyptAir lilisema kuwa lilikuwa likisitisha safari za ndege kwenda na kutoka Khartoum kwa saa 72.

Chanzo: Bbc