Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maseneta wa Nasa Wamwondoa Malala Kama Naibu Kiongozi wa Wachache

1b4143e2901dd6ab Maseneta wa Nasa Wamwondoa Malala Kama Naibu Kiongozi wa Wachache

Wed, 24 Mar 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Maseneta 18 walitia saini mchakato wa kumbandua seneta huyo katika nafasi hiyo

- Malala anatuhumiwa kwa madai ya utovu wa nidhamu na ufisadi katika uchaguzi mdogo uliomalizika hivi karibuni wa Matungu

Seneta wa Kakamega Cleophas Malala ameondolewa kama Kiongozi wa Wachache wa Seneti katika mkutano wa Kikundi cha Bunge la Seneti la NASA.

Seneta wa Kilifi Stewart Madzayo wa ODM alichaguliwa kuchukua nafasi ya Malala wakati wa mkutano uliofanyika kwenye majengo ya Bunge.

Muungano wa National Super Alliance (NASA) uliandaa kikao cha Bunge la Seneti ambapo Seneta wa Kakamega Cleophas Malala aliondolewa kama naibu wa Kiongozi wa Wachache wa Seneti.

Mkutano huo ulijiri wakati wa kumekuwepo na tofauti baina ya wanachama wa NASA kuhusu hatima ya seneta huyo ambaye amepata uungwaji mkono wa maseneta kutoka Wiper, ANC, na Ford Kenya.

Ombi la kuondolewa kwake tayari limesainiwa na Maseneta wa ODM ila bado halijatiwa saini na maseneta kutoka vyama vingine ambao walichaguliwa au kuteuliwa chini ya mwavuli wa Nasa katika uchaguzi mkuu wa 2017.

Ripoti zinaonyesha kwamba Kiongozi wa Wachache James Orengo alifanya mkutano ambapo aliidhinisha kuondolewa kwa naibu wake.

Seneta huyo wa Kakamega ni mshirika wa karibu wa Musalia Mudavadi wa ANC ambaye hivi karibuni alitengana na uomgozi wa ODM.

Masaibu ya Malala na uongozi wa ODM yaliongezeka wakati alipomuunga mkono mgombea wa ANC katika uchaguzi mdogo wa Matungu.

Maseneta 28 wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo ambao kaulimbiu yake kuu ni kuamua hatima ya Malala kama naibu wa kiongozi wa wachache wa Seneti.

Seneta wa Taita Taveta Johnes Mwaruma anaonekana kupendekezwa kama chaguo bora kuziba pengo la Malala.

Tofauti za wanachama wa zamani wa muungano wa Nasa ulianza baada ya baadhi ya viongozi kukataa kujitokeza katika kiapo cha utata cha kinara wa chama cha ODM Raila Odinga kuwa Rais wa Watu.

Tangu wakati huo, Raila, Musalia, Kalonzo na Wetangula wamelaumiana hadharani huku kila upande ukimtuhumu mwingine kwa usaliti na kutotimiza ahadi.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke