Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Masaibu ya UDA: Jamaa ataka kumpokonya DP Ruto nyama mdomoni

2f14f7853f1b945a Masaibu ya UDA: Jamaa ataka kumpokonya DP Ruto nyama mdomoni

Sat, 24 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Noor alisema wandani wa DP Ruto walichukua UDA kutoka kwa PDR bila kufuata sheriaAmeandikia jopo la kutatua mizozo ya vyama akitaka Muthama, Khalwale na Maina kuytimuliwa kutoka nyadhifa za chamaHali kama hiyo ilimpata Ruto awali ambapo alitoka ODM na kuingia UDM lakini masaibu yakaingia na kumlazimu kuunda URPJamaa amekimbia mahakamani akitaka jopo la kutatua mizozo ya kisiasa kubadili uongozi wa chama cha United Democratic Alliance (UDA).

Aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho kabla ya kubadilishwa jina na kuwa UDA Mohamed Abdi Noor amedai kuwa njia za kisheria hazikufuatwa wakati wa kupata uongozi mpya.

Noor aliandikia jopo la kutatua mizozo ya vyama akitaka kurudishiwa wadhifa wake kwa kuwaondoa Johnstone Muthama ambaye sasa ni mwenyekitim naibu mwenyekiti Boni Khalwale na katibu Veronica Maina.

UDA ilikuwa PDR hapo awali kala ya mabadiliko na Noor anasema maafisa wa chama walioidhinisha mabadiliko hayo hawakuwa halali.



Read also

Uchunguzi wa Maiti kwa Watoto 2 Aliodaiwa Kuwauwa Masten Wanjala Wafanywa



Aliambia jopo hilo kuwa msajili wa vyama humu nchini alikosea kwa kuidhinishwa kubadilishwa kwa PDR kuwa UDA bila katiba ya chama hicho kufutwa.

Alisema mabadiliko hayo yalitiwa sahihi na aliyekuwa katibu wa PDR Mohamed Sahal wakati ambapo alikuwa akitumikia hatua za kinidhamu.

"Katibu wa chama wakati huo alikuwa pia ni mtumishi wa uma na hivyo alikuwa akihudumu kama katibu kinyume cha sheria kwa mujibu wa kipengee cha 12 kwenye sheria kuhusu vyama na hivyo hatua yake haikubaliki," alisema Noor.

Naibu mwenyekiti wa UDA Bonny Khalwale hata hivyo amesema hatua ya Noor ni njama ya mahasimu wao kuangusha UDA.

Alisema bahati yao ni kuwa waliwahusisha wanasheria katika kuchukua PDR na kuifanya UDA.

"Nashukuru Mungu kuwa kikosi chetu cha wanasheria kilihakikisha kuwa kila kitu iko sawa kutoka kuwa PDR mpaka UDA," alisema Khalwale.



Read also

Magazeti Ijumaa: Moses Kuria Afukuzwa PEP, UDA Yakumbwa na Mzozo

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

azama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke