Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametoa amri ya watu kutotoka nje ya Wilaya mbili ambazo mlipuko wa virusi vya Ebola ulianzia, kwa muda wa siku 21.
Museveni amesema kwamba serikali inafanikiwa kudhibithi maambukizi ya ebola nchini humo. Amri hiyo itatekelezwa kadi Disemba tarehe 17. Awali kulikuwa na amri kama hiyo ya siku 21 kuanzia Oct 15, na ilimalizika Nov 5.
Yoweri Museveni ameongeza kwamba hatua hiyo imechukuliwa ili kuhakikisha kwamba mafanikio ambayo yamepatikana kufikia sasa katika kukabiliana na mlipuko wa Ebola, yanaendelea na kuhakikisha kwamba hakuna kabisa maambukizi ya virusi hivyo nchini humo katika muda wa siku chache.
Serikali imesema kwamba hakuna maambukizi mapya yameripotiwa katika wilaya hizo mbili
Watu 141 wamethibitishwa kuambukizwa Ebola nchini Uganda. 55 wamefariki tangu Septemba 20 mlipuko uliporipotiwa. Hakuna chanjo dhidi ya virusi vya Ebola aina ya Sudan vinavyoripotiwa Uganda.